Consecration service Of St. Mary's Menza Mwenye
on 15th sept 2024 by George Konde
Askofu wa Jimbo la Mombasa Daktari Alphonce Mwaro Baya, Rais wa Umaki, kasisi Martha Mwaro, pamoja na makasisi wameungana na waumini kushiriki katika ibada ya kuweka wakfu kanisa la mtakatifu Maria Menza-Mwenye lililoko Lunga-Lunga Kaunti ya Kwale.
Ujenzi wa kanisa la Mtakatifu Maria ni mradi uliofadhiliwa, kusimamiwa na kufanikishwa na ofisi ya umaki Jimbo la Mombasa. Hii ni hatua kubwa ya kimishonari ili kueneza injili mashinani. Haya ni baadhi ya maono ya ofisi ya umaki kujenga makanisa katika Kaunti za Jimbo la Mombasa ikiwemo Kaunti ya Mombasa,Kwale na Kilifi.
Our Mission Statement ( A Transforming Diocese For Holistic)
Askofu Alphonce amefafanua maana ya wakfu kuwa ni kuenda nyumbani kwa bwana, kukamilisha maono, na kuwa, wakristo ni nyumba ya sala.
Tunatoa pongezi na shukrani zetu za dhati kwa umoja wa kina mama Jimbo la Mombasa, wote waliotoa michango yao kifedha, kimaombi na hata kimawazo na maoni, wote waliofanikisha ujenzi wa kanisa hili, Kasisi Ernest Ndune pamoja na waumini wa kanisa la Mtakatifu Maria Menza-Mwenye kwa ushirikiano wao na waandalizi wa shughuli hii.RegionAnglican Development Services Pwani RegionThe Anglican Church of KenyaArchbishop Jackson Ole SapitAnglican CommunionNews ServiceGREEN Anglicans
Diocesan Bishop
Vicar General
Administrative secretary